TIMU YA KIRAFIKI KATI YA CHUO CHA JEMA NA FRESHERIES NYEGEZI WAMALIZIKA

Leo kulikuwa na mpira wa miguu kati ya timu ya chuo cha JEMA na chuo cha Fresheries. katika mechi hiyo wenyenji walikuwa ni Fresheries Nyegezi.

katika mpira huo wachezaji wote wamecheza  mpira mzuri na hakuna timu iliyolalamika.

kwa upande mwingine wanafunzi wa chuo cha JEMA  wamefurahishwa na namna utawala unavowapa sapoti katika matukio ya Michezo.

Kwa upande wa chuo unawapongeza wachezaji wa mpira kwa kujitoa kwa hali na mali wakiwa uwanjani licha ya kuwa mvua ilinyesha na ikalazimika refa kusimamisha mpira kwa muda.

Matokeo ni kwamba wenyenji waliibuka kwa magoli mawili dhidi ya goli moja walilofunga wageni wa mechi hiyo yaani JEMA.

Powered by JIT Team